×
TAFUTA
Mahali Salama pa Kuchunguza Maswali
 jinsi unavyoweza kumjua Mungu
Kuwepo kwa Mungu

Mungu yuko wapi katika nyakati ngumu?

Umewahi kuuliza, “Mungu uko wapi?” Ni nini hasa unaweza kumtegemea Mungu?

WhatsApp Share Facebook Share Twitter Share Share by Email More PDF

Sikiliza makala hii:

Ni kwa kiwango gani tunaweza kumtegemea Mungu ili atusaidie? Je, ni kweli ni Mungu tunayeweza kumgeukia kabisa…katika nyakati za shida na hata nyakati za utulivu?

Mungu ni nani?

Mungu ndiye Muumba wa ulimwengu ambaye anatamani sana tumjue. Ndiyo maana sote tuko hapa. Ni tamaa yake kwamba tumtegemee na tushiriki Nguvu zake, Upendo, Haki, Utakatifu na huruma zake. Kwa hiyo anawambia wote wanaotaka. “Njooni Kwangu”.

Tofauti na sisi, Mungu anajua nini kitatokea kesho, wiki ijayo, mwaka ujao, muongo ujao. Anasema, “mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; niutangazae mwisho kutoka mwanzo;”1 Anajua kitakachotokea duniani. Muhimu zaidi, anajua kitakachotokea katika maisha yako na anaweza kuwapo hapo kwa ajili yako, kama umechagua kumujuisha Yeye kwenye maisha yako. Anatuambia kwamba anaweza kuwa, “kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.”2 Lakini ni lazima tufanye jitihada ya kweli kumtafta. Anasema, “Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote”3

Hiyo haimaanishi kwamba wale wanaomjua Mungu wataepukana nyakati ngumu. Kwamb hawangepitia. Wakati vita au mlipuko wa ugonjwa yanaposababisha kuteseka na kifo, wale wanaomjua Mungu watahusika katika mateso hayo pia. Lakini kuna amani na nguvu ambayo uwepo wa Mungu hutoa. Mfuasi mmoja wa Yesu Kristo alisema hivi: “Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi;”4

Ukweli anatuambia kwamba tutapitia matatizo katika maisha. Hata hivyo, kama tutapitia uku tunamjua Mungu, tutayashuruhisha tukiwa na mtazamo tofauti na kwa nguvu ambayo si yetu wenyewe. Hakuna tatizo ambalo ni kubwa la kumshinda Mungu. Yeye ni mkubwa kuliko matatizo ambayo yanaweza kutupata, na atujaacha peke yetu kukabiliana nayo.

Neno la Mungu linatuambia, “BWANA ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.”5 na “BWANA yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu. Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.”6

Yesu Kristo aliwaambia wafuasi wake kwa maneno haya ya faraja: “Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu; lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi; bora ninyi kuliko mashomoro wengi.”7 kama kweli utamugeukia Mungu, atakujali kuliko mtu yeyote anayeweza kukujali, na kwa njia ambayo hakuna mwingine awezaye.

Mungu na Utashi wetu

Mungu amemuumba mwanadamu akiwa na maamuzi ya kuchagua. Hii inamaanisha kuwa hautasukumwa kuwa na uhusiano naye. Ameturuhusu kumkataa na kutenda maovu pia. Anaweza kutulazimisha tumpende. Anaweza kutulazimisha kuwa wema. Lakini basi tungekuwa na uhusiano wa aina gani Naye? kama kulazimishwa, utii uliodhibitiwa kabisa, Usingekuwa uhusiano hata kidogo. Lakini badala yake alitupa utu wa hiari.

Kwa kawaida, tunalia kutoka ndani kabisa ya nafsi zetu..."Lakini Mungu, ungewezaje kuruhusu jambo la ukubwa huu kutokea?"

Tungetaka Mungu atendeje? Tungetaka atawale matendo ya watu? Katika kesi ya kushughulikia shambulizi la kigaidi, ni idadi gani inayokubalika ya vifo ambayo Mungu angeruhusu?! Tunaweza kujisikia vizuri iwapo Mungu angeruhusu mauaji ya mamia? Au tungekubali Mungu aruhusu kifo cha mtu mmoja? Lakini kama Mungu angezuia mauaji ya hata ya mtu mmoja, hapo sio tena uhuru wa kuchagua. Watu uchagua kumkataa Mungu, na kwenda katika njia zao wenyewe na kufanya vitendo vya kutisha dhidi ya wengine.

Sayari hii si mahali salama. Mtu anaweza kutupiga risasi. Au tunaweza kugongwa na gari. Au huenda tukalazimika kuruka kutoka katika jengo lililoshumbliwa na magaidi. Au idadi ya mambo ambayo huenda yakatokea kwetu katika mazingira magumu yanaoitwa Dunia, mahali ambapo mapenzi ya Mungu hayatafutwi kila mahala. Bado, Mungu hayuko kwenye rehema za watu, lakini kinyume chake. Tuko kwenye rehema zake, kwa bahati nzuri. Huyu ni Mungu alieumba ulimwengu pamoja na nyota zisizohesabika, kwa kusema tu maneno haya, “Na iwe mianga katika anga;”8 Huyu ni Mungu asemaye “anatawala juu ya mataifa.”9 Yeye hana kikomo katika nguvu na hekima.

Ingawa matatizo yanaonekana kuwa magumu kwetu, tunaye Mungu mwenye uwezo wa ajabu anayetukumbusha, “Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?”10 Mara nyingine yeye anaweza kuheshimu uhuru wa mwanadamu mzambi, na bado akawa anamletea mapenzi yake. Mungu alisema wazi “Shauri langu litasimama, nami nitatimiza makusudi Yangu yote.”11 na tunaweza kupata faraja kutoka kwake iwapo tumetoa maisha yetu kwake “Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.”12

Mungu Yuko Wapi Tunapomkataa?

Wengi wetu--hapana, sote – tukichagua muda wa kushikamana na Mungu na njia zake. Kulinganishwa na wengine, kwa hakika tukijilinganisha na gaidi or jambazi, tunaweza kujiona kuwa watu wenye heshima, wanaopenda watu. Lakini kwa uaminifu wa kweli wa mioyo yetu, kama tunatakiwa kukutana na Mungu, tungefahamu dhambi zetu. Tunapoanza kuongea na Mungu katika maombi, je, hatushikiki, na kutetemeka kwa hisia zetu kwamba Mungu anajua mawazo yetu, matendo na ubinafsi wetu? Tuna … kwa maana maisha na matendo yetu yanatuweka mbali na Mungu. Mara nyingi tumeishi kana kwamba tunaweza kuendesha maisha yetu vizuri bila yeye. Biblia inasema kwamba “Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.”13

Matokeo yake? Dhambi yetu imetutenganisha na Mungu, na inaathiri zaidi ya maisha haya. Adhabu ya dhambi zetu ni kifo, au kutengwa na Mungu milele. Hata hivyo, Mungu ametuandalia njia ya kusamehewa na ya kumjua.

Mungu Utupa Upendo Wake

Mungu alikuja duniani kutukomboa. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”14

-Mungu anajua maumivu na mateso tunayokumbana nayo katika ulimwengu huu. Yesu aliacha enzi na usalama wa nyumba yake, na akaingia katika mazingira magumu tunamoishi. Yesu alichoka, alijua njaa na kiu, alishindana na shutuma kutoka kwa wengine na alitengwa na familia na marafiki. Lakini Yesu alipitia changamoto kubwa zaidi ya magumu ya kila siku. Yesu, Mwana wa Mungu katika umbo la mwanadamu, kwa hiari alichukua dhambi zetu na akatulipia deni la mauti. “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu;”15 Alipitia mateso, akifa kifo cha polepole, cha kufedhehesha cha kukosa hewa juu ya msalaba, ili sisi tupate kusamehewa.

Yesu aliwaambia wengine kabla ya wakati kwamba angesulubishwa. Alisema kwamba siku tatu baada ya kifo chake angefufuliwa, akithibitisha kwamba yeye ni Mungu. Hakusema angezaliwa upya siku moja. (Nani angejua kama kweli alifanya hivyo?) Alisema siku tatu baada ya kuzikwa angejionyesha akiwa hai kimwili kwa wale walioona akisulubishwa. Siku hiyo ya tatu, kaburi la Yesu lilipatikana tupu na watu wengi walishuhudia kumuona akiwa hai.

Mungu Anatualika Tuwe Naye Mbinguni

Sasa anatupatia uzima wa milele. Hatuwezi kupata kwa fedha. Ni zawadi anayotoa Mungu kwetu, ambayo tunaipokea ambapo tunamuomba yeye aingie kwenye maisha yetu. “bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”16 Kama tukitubu dhambi zetu na kumrudia tena Mungu, tunaweza kupata uzima wa milele kupitia Yesu Kristo. Ni rahisi. “Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.”17 Anataka kuingia kwenye maisha yetu.

Vipi kuhusu mbinguni? Biblia inasema kwamba Mungu “ameweka umilele ndani ya mioyo ya wanadamu.”18 Labda hiyo inamaanisha kwamba tunajua mioyoni mwetu jinsi ulimwengu mzuri unatakiwa uwe. Vifo vya wanadamu vimetusawishi tuone kuna tatizo kubwa mahala katika maisha haya na katika ulimwengu huu. Sehemu fulani ndani ya nafsi zetu, tunajua kunasehemu nzuri zaidi ya kuishi, pasipo na matatizo na maumivu yenye kuhuzunisha moyo. Kwa hakika, Mungu anamahali pazuri pakutupatia. Utakuwa ni mfumo tofauti uliokamilika ambapo mapenzi yake yatafanyika kila wakati. Katika ulimwengu huu, Mungu atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena;19 Na Mungu, kwa Roho wake, atakaa ndani ya watu kwa namna ambayo hawatatenda dhambi tena.20

Matukio ya migogoro ya ghafla au mashambulizi ya kigaidi na matukio ya kutosha ya kutisha. Ukikataa uhusiano wa milele na Mungu, ambavyo alimtoa Yesu kwako, itakuwa ni mbaya zaidi. Sio tu katika mwanga wa uzima wa milele, lakini hakuna uhusiano unaolinganishwa na kumjua Mungu katika maisha haya. Yeye ndiye kusudi letu maishani, ni chanzo chetu cha faraja, hekima yetu katika nyakati za kutatanisha, nguvu na tumaini letu “Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini.”21

Imesemwa na watu fulani kwamba Mungu ni mkongojo tu. Lakini kuna uwezekano kwamba Yeye ndiye pekee anayetegemewa.

Yesu alisema, “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.”22 Kwa wale wanaomtegemea Yesu katika wa maisha yao, Anasema ni kama kujenga maisha yako juu ya Mwamba. Migogoro yoyote inayokushambulia katika maisha haya, Anaweza kukuweka imara.

Mungu yuko wapi? Anaweza Kuingia Katika Maisha Yako

Unaweza kupokea Yesu aje katika maisha yako sasa. “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;”23 Ni kwa njia ya Yesu Kristo kwamba tunaweza kumrudia Mungu. Yesu alisema, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”24 Yesu akasema, “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.”25

-Sasa hivi unaweza kumwomba Mungu aingie katika maisha yako. Unaweza kufanya hivyo kupitia maombi. Maombi yanamaanisha kuzungumza kiuaminifu na Mungu. Kwa wakati huu unaweza kumwita Mungu kwa kumwambia jambo kama hili kwa uaminifu:

"Mungu nimejitenga na wewe moyoni mwangu, lakini nataka kubadilisha hilo, nataka kukujua. Nataka kumpokea Yesu Kristo na msamaha wake maishani mwangu. Sitaki tena kutengwa nawe tena. Uwe Mungu wa maisha yangu kuanzia leo na kuendelea. Asante Mungu."

Je, sasa hivi umemwomba Mungu kwa dhati maishani mwako? Kama umefanya hivyo, unatakiwa uangalie mbele. Ahadi ya Mungu ni kufanya maisha yako ya sasa kuwa ya kuridhika zaidi kwa kumjua.26 Mungu yuko wapi? Amehaidi kufanya makao ndani yako.27 naye anakupa uzima wa milele.28

Haijalishi kinachotokea katika ulimwengu unaokuzunguka, Mungu anaweza kuwa upande wako. Ijapokuwa watu hawafuati njia za Mungu, Mungu anaweza kuchukua mazingira magumu na akaleta mpango wake. Mungu anadhibiti matukio yote ya ulimwengu. Kama ni Mungu wako, sasa unaweza kupumzika katika ahadi yake ya, “kuwa hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”29

Yesu Kristo alisema, “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo Mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.”30 ameahidi hatatupungukia kabisa, wala kutuacha kabisa.”31

 Nilimpokea Yesu maishani mwangu (ujumbe muhimu unafuata)…
 Ninaweza kutaka kumuuliza Yesu maishani mwangu, tafadhali eleza hili kikamilifu zaidi…
 Nina swali…

[na Dkt. Marilyn Adamson]

Maelezo ya chini: (1) Isaya 46:9 (2) Zaburi 46:1 (3) Yeremia 29:13 (4) 2Wakorintho 4:8-9 (5)Nahumu 1:7 (6) Zaburi 145:18-19 (7) Mathayo 10:29-31 (8) Mwanzo 1:14 (9) Zaburi 47:8 (10)Yeremia 32:27 (11) Isaya 46:11 (12)Yakobo 4:6 (13) Isaya 53:6 (14) Yohana 3:16-17 (15)1Yohana 3:16 (16) Warumi 6:23 (17) 1Yohana 5:12 (18) Mhubiri 3:11 (19) Ufunuo 21:4 (20)Ufunuo 21:27; 1Wakorintho 15:28 (21) Zaburi 34:8 (22) Yohana 14:27 (23)Yohana 1:12 (24) Yohana 14:6 (25) Ufunuo 3:20 (26) Yohana 10:10 (27) Yohana 14: 23 (28) 1Yohana 5:11-13 (29) Warumi 8:28 (30) Yohana 14:27 na 16:33 (31) Waebrania 13:5


SHIRIKISHA WENGINE
WhatsApp Share Facebook Share Twitter Share Share by Email More