×
TAFUTA
Mahali Salama pa Kuchunguza Maswali
 jinsi unavyoweza kumjua Mungu
Kuwepo kwa Mungu

Kuunganishwa na Mungu

Dini kubwa ulimwenguni na imani zao…

WhatsApp Share Facebook Share Twitter Share Share by Email More PDF

Sikiliza makala hii:

Sote tunataka kuwa na mafanikio katika maisha yetu, kwa ufahamu huo tunafanya sawa. Je, kuhusu dini kubwa za ulimwenguni? Kuna cha ziada ndani ambacho kinaweza kutupa uzito na mwelekeo?

Ifuatavyo tunaangalia dini kubwa za ulimwenguni… Uhindu, Enzi Mpya, Ubudha, Uislamu, na Ukristo. *Kuna maelezo mafupi kwa kila moja, maoni yao kwa Mungu, na kila mtu kile anachoweza kupata kupitia hiyo dini. Mwishoni tutaelezea ambavyo mafundisho ya Yesu yanatofautiana na dini hizo kubwa.

*Hizi dini zinatofautiana katika imani. Maelezo yaliyotolewa hapa yanalenga katika msingi wa imani wa kila dini. Dini nyingine kubwa kama Uyahudi, inaweza kufanyiwa mdahalo, lakini kwa ufupi, tumechagua hizi.

Dini Kihindu na imani zake

Illustration of Hinduism with arrows all pointing in various directions to show infinite manifestations of God.Wahindu wengi huabudu Kiumbe kimoja cha umoja wa mwisho (Brahman) kupitia uwakilishi usio na mwisho wa miungu na miungu ya kike. Miungu hii mbalimbali inakuwa imeumbika ndani ya sanamu, mahekalu, mito, wanyama, n.k.

Wahindu wanaamini hali walionazo sasa zimechangiwa na matendo yao ya maisha ya zamani. Kwahiyo dini ya kihindu hutoa ufafanuzi juu ya mateso na maovu katika maisha haya. Kama tabia ya mtu ya zamani ilikuwa imegubikwa na uovu, maisha yake ya sasa yanaweza kuwa magumu. Kama kupitia Maumivu, magonjwa, umasikini au maafa kama mafuriko anayoistaili mtu huyo kwa sababu ya makosa ya matendo yake, kawaida utoka katika maisha ya zamani.

Lengo la dini ya Kihindu ni kuwa huru kutoka kwenye sheria za karma…kuwa huru kutokana na kuzaliwa upya mara kwa mara. Nafsi pekee ndiyo inayohusika ambayo siku moja itakuwa huru kutoka kwenye mzuko wa kuzaliwa upya na kupumuzika.

Dini ya Kihindu humuruhusu mtu kuchagua ni kazi ipi ya kufanya kuelekea ukamilifu wa kiroho. Kuna njia tatu za kumaliza mzunguko wa karma: 1. Ujitolee kwa upendo kwa miungu yoyote ya Kihindu; 2. Kuza ujuzi kupitia kutafakari kwa Brahman… kutambua kwamba hali katika maisha sio halisi, kwamba ubinafsi ni dhambi na Brahman pekee ndiye halisi; 3. Kuwa wakfu kwa ibada na sherehe mbalimbali za kidini.

Enzi Mpya na imani zake

Illustration of New Age Spirituality, showing arrows interconnecting in a circle, to illustrate that a person becomes their own God.Dini ya Enzi Mpya inakuza maendeleo ya nguvu au uungu wa mtu mwenyewe. Tunapo rejerea katika uungu, mfuasi katika aina hii ya kiroho haongelei juu ya Umungu, au Mungu wa binafsi ambaye aliumba ulimwengu, badala yake wanausisha ukuu uliondani mwao wenyewe. Mtu akifanikiwa kukua kiroho atajiona kuwa yeye ni mungu, katika mazingira, ama ulimwenguni. Kwa kweli, kile ambacho unakiona, kusikia, kuisi au kufikilia kinapaswa kuzingatiwa kuwa cha kimungu.

Utamaduni wa hali ya juu sana, Dini ya Enzi Mpya ni mkusanyiko wa mila za kale za kiroho, zinazofundishwa na safu nyingi za wazungumzaji, vitabu and semina. Dini hii inakubaliana na miungu mingi na miungu ya kike, kama wahindu. Dunia utazamwa kama chanzo cha hali zote za kiroho na kuwa ina akili, hisia na uungu wake. Lakini kushinda kote ni ubinafsi. Binafsi ni mwanzilishi, mtawala na mwenye nguvu juu ya vyote. Hakuna ukweli nje ya kile mtu anachoamua.

Dini ya Enzi Mpya ufundisha mafumbo ya mashariki na mbinu za kiroho, kimetafizikia na ujuzi wa kiakili kama mazoezi ya kupumua, kuimba, kupiga ngoma, kutafakari ili kukuza ufahamu na uungu wa mtu mwenyewe.

Kitu chochote kisicho chema ambacho mtu upitia (kushindwa, uzuni, hasira, ubinafsi, maumivu) huchukuliwa kama udanganyifu. Wanajiamini wenyewe kuwa wanamamlaka kamili katika maisha yao, hakuna ambacho hakikosawa kwenye maisha yao, iwe shida ama maumivu. Hatimaye mtu ukua kiroho katika kiwango cha hakuna kitu chenye ukweli nje yake mwenyewe. Mtu anakuwa mungu, anaumba ukweli wake mwenyewe.

Wabudha na Imani yao

Illustration of Buddhism, with a universal sign of nill, a circle with a slanted line through it, to illustrate that Buddhists do not believe in any God.Wabudha hawaabudu miungu au Mungu. Watu nje ya ubudha wanafikiri kuwa wabudha wana mwabudu Budha. Hata hivyo, Budha (Siddhartha Gautama) hajawai kujiita kuwa yeye ni mungu, lakini wabudha wanaona kuwa amefikia hatua ambayo na wao wanafikilia kufikia, ambayo ni nuru ya kiroho na pamoja na uhuru unaotoka katika mzunguko unaoendelea wa maisha na kifo.

Wabudha wengi wanaamini kuwa mtu ana nafasi kubwa ya kuzaliwa upya, ambayo haipingiki pamoja na mateso. Mbudha anatafta kukomesha kuzaliwa upya. Wabudha wanaamini kuwa ni tamaa ya mtu, chuki na udanganyifu unaosababisha kuzaliwa tena. Kwahiyo, dhumuni la wabudha ni kutaka moyo wa mtu na kuachana na matamanio yanayopelekea mwili kuwaka tamaa na kushikamana na tamaa hiyo.

Wabudha hufuata kanuni za kidini zinazo muelekeza mtu binafsi anavyoweza kuijizuia, kufunga na jinsi kufanya tafakari yake kikamilifu. Wakati wabudha wanatafakari sio sawa na kuomba au kujielekeza kwa Mungu, ni zaidi ya nidhamu binafsi. Kupitia mazoezi ya kutafakari mtu ufikia hatua ya kutoa nje tamaa ya mwili (Nirvana).

Dini ya wabudha hutoa kitu ambacho ni sawa na dini nyingine kuu kama nidhamu, maadili na maagizo ambayo mtu anaweza kutaka kuishi kwayo.

Uislamu na imani zake

Illustration of Islam, with one arrow pointing up to a transcendent God, to illustrate the relationship with God is one serving that God.Waislamu wanaamini kuwa Mungu mmoja mwenyezi, anayeitwa Allah, ambaye ni mkuu zaidi na asiye na kikomo kutoka katika utu wa mwanadamu. Allah anatazamwa kama muumba ulimwengu na chanzo cha mazuri na mabaya. Kila kinachotokea ni mapenzi ya Allah. Ni mwenye nguvu na ni hakimu mkali, ni mwenye huruma kwa wanaomfuata kutegemea matendo mema ya maisha yao na ibada kidini. Wafuasi wakiwa na uhusiano na Allah ndio kumtumikia.

Ingawa katika uislamu wanaheshimu manabii wengi. Muhammad anaaminiwa kuwa ndie nabii wa mwisho na maneno yake na mwenendo wake ni mamlaka ya mtu huyo. Kuwa Muislamu lazima ufuate nguzo tano za uislamu: 1. Jenga imani kwa Mwenyezi Mungu (Allah) na Mtume Muhammad; 2. Sali swala tano kwa kiarabu kwa siku; 3. Wape masikini vitu; 4. Mwezi mmoja kila mwaka funga kula chakula, kunywa maji, kumjua mwanamke na kuvuta sigara kutoka mawio mpaka machweo ya jua; 5. Kwenda hija uko Makka walau mara moja kwenye maisha ya mtu. Iwapo muislamu amezingatia haya kwa uaminifu akifa anamatumaini yakuingia peponi la sivyo atateseka milele kuzimu.

Kwa watu wengi, uislamu unalingana na matarajio kuhusu dini na uungu. Uislamu unafundisha kwamba, mungu mmoja mkuu, ambaye anaabudiwa kwa matendo mema na taratibu za kidini zenye nidhamu. Baada ya kufa mtu hutuzwa au uadhibiwa kutokana kutii kwao katika dini. Waislamu wanaamini kutoa uhai wako kwa ajili ya Allah ni njia yenye uhakika ya kuingia peponi.

Ukristo na imani zake

Illustration of Christianity, with an arrow of God reaching down to an arrow of a person being able to connect with God.Wakristo wanaamini katika Mungu mmoja wa milele ambaye ndiye muumbaji wa vyote. Wanamuona Mungu kuwa mwenye Upendo ambaye anampa kila mtu uhusiano wake binafsi katika maisha haya.

Katika maisha yake hapa Duniani, Yesus Kristo hakujitaja kuwa yeye ni nabii aliyeteuliwa na Mungu au mwalimu aliyeinuliwa kufundisha. Badala yake, Yesu alidai kuwa yeye ni Mungu katika mwanadamu, “Mungu pamoja nasi”. Alifanya miujiza, alisamehe watu dhambi zao na akasema yeyote atakaye muamini atapata uzima wa milele.

Wafuasi wa Yesu huona Biblia kuwa ni Neno la Mungu kwa wanadamu. Kwa kuongezea historia ya maisha ya Yesu na miujiza, Biblia imefunua utu wake, upendo na ukweli wake, na jinsi mtu anavyoweza kumjua Mungu na kuwa na mahusiano naye, hata akamfanya rafiki.

Wakristo wanaamini kwamba watu wote ni waovu, pamoja na wao wenyewe. Wanamuona Yesu kama Mwokozi wao, kama Masihi alietabiriwa na manabii wote katika Agano la Kale, katika Biblia. Wanaamini Yesu Kristo, nje ya upendo wake kwetu, alilipa deni la dhambi kwa wanadamu wote alipokufa pale msalabani. Baada ya siku tatu, alifufuka kutoka katika wafu kama alivyohaidi, kudhibitisha uungu wake.

Dini hizi kubwa zinatofautianaje?

Kwa kuangalia mifumo ya dini hizi kubwa na maono yao kwa Mungu, tunapata utofauti mkubwa sana:

  • Wahindu hukubali wingi wa miungu na miungu ya kike.
  • Wabudha wanasema hakuna mungu.
  • Wafuasi wa Enzi mpya wanaamini wao ni Mungu.
  • Waislamu wanaamini katika Mungu mwenye nguvu lakini asiyejulikana.
  • Wakristo wanaamini kwamba kuna Mungu mwenye upendo ambaye alituumba ili tumjue.

Dini hizo zote zinamuabudu Mungu mmoja? Hebu tuzingatie hilo. Dini ya Enzi mpya inafundisha kwamba kila mtu anapaswa kuzingatia tu ufahamu wa ulimwengu, lakini inatakiwa muislamu ajitoe kwa Mungu wao mmoja. Wahindu wajitoe kwa miungu na Wabudha wathibitishe kuwa kuna Mungu.

Kila dini inahitaji nini?

Dini kubwa za ulimwenguni (Uhindu, Enzi Mpya, Ubuddha, Uislamu, Ukristo) zina upekee katika uitaji wake.

Photo of a smiling young man to illustrate that in Christianity there is not the burden to earn God's acceptance.Dini nyingi za ulimwengu umumiliki mtu na kumuendesha apate ukamilifu rohoni.

Kwa dini ya wahindu, mtu anajibidiisha kupata ukombozi kutoka kwa karma. Kwa dini ya Enzi mpya, mtu anafanyia kazi uungu wake mwenyewe. Kwa dini ya budha, mtu binafsi anajibiisha kukimbia tamaa ya mwili. Na katika uislamu, mtu anatakiwa afuate sheria za dini kwa ajili ya kuingia peponi baada ya kifo.

Dini zote zinashughulikia shida moja.

Sote tunafahamu mapungufu ya kibinafsi na hitaji la kuwa bora zaidi. Hili ndilo linalopelekea kuundwa kwa dini.

Pia tunataka kujisikia amani, kuridhika na kuwa na nguvu za ndani. Na kwa hivyo tunahamia kwenye mazoea kama kutafakari, mila ya kidini, vitabu vya kujisaidia, kufunga, maombi, dhabihu za kibinafsi, kuiji, n.k.

Tunatumaini haya yataongeza wema wetu wa ndani na kufanya marekebisho kwa dhambi zetu.

Wakati wakijitahidi kupata elimu, Buddha hakuwahi kudai kutokuwa na dhambi. Muhammad pia alikiri kwamba alikuwa anahitaji msamaha. "Haijalishi ni wenye hekima kiasi gani, haijalishi walikuwa na karama kiasi gani, haijalishi manabii wengine, wakuu, na walimu wangekuwa na ushawishi kiasi gani, walikuwa na uwepo wa akili kujua kwamba hawakuwa wakamilifu kama sisi wengine."1

Sadaka katika dini mbalimbali

Katika dini nyingi, unaona aina fulani ya dhabihu inayohitajika kulipia dhambi.

man meditating in worshipKatika Uhindu, moto mtakatifu unaweza kutumika kushinda dhambi, mateso na shida. Katika dini nyingine ni kawaida kuhitaji saa katika maombi au kutafakari mara nyingi kwa siku; vipindi vya kufunga; dhabihu za kifedha; ija ya muda mrefu.

Nabii Isaya ni nabii aliyeheshimiwa katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu. Badala ya kuangaika kulipia dhambi zetu, Isaya aliandika kwamba atakuja Mwokozi ambaye yeye mwenyewe atalipa deni la dhambi za wanadamu wote.

“Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu [dhambi] yetu sisi sote.”2

Yesu Kristo alijitambulisha kuwa ndiye Mwokozi ambaye Isaya alisema habari zake “… Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”3

Yesu aliwaambia wafuasi wake kuwa atautoa uhai wake “…imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.”4

Msamaha wa dhambi

Hakika, Yesu alipigwa mijeledi, akapigwa, taji la ndefu la miiba likibanwa kichwani mwake, kisha mikono na miguu yake ikagogomelewa msalabani, ambapo aliachwa hapo mpaka kufa, akifa kwa hiari yake mwenyewe kwa ajili yetu.

Nabii Isaya aliandika, Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu…alimwaga nafsi yake hata kufa …sadaka ya hatia…alichukua dhambi za watu wengi,”5

Biblia inasema, “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu;”6

Dhambi zetu zililipwa na Yesu msalabani. Sasa anatupa msamaha kamili na atatukaribisha katika raha yake.

Maisha baada ya kifo

Katika maisha yake yote ya hadharani, maelfu ya watu walimfuata Yesu, alipofanya miujiza isiyo na idadi, uponyaji wa wagonjwa, kufanya viwete watembee, vipofu kupata kuona, kuwalisha watu zaidi ya 5,000.

Tofauti na viongozi wengine wa kiroho, Yesu alisema yeye mwenyewe kuwa atauhukumu ulimwengu, atawasamehe watu dhambi zao, na kuwapa uzima wa milele, atawajibu maombi yao… kwa ajili ya Utukufu wa Mungu pekee. Tena na tena alijitambulisha kuwa yeye ni sawa na Mungu, iliyopelekea kusulubiwa kwake.

Hata hivyo, Yesu pia alitoa uthibitisho wake wa mwisho wa uungu wake, akisema atazikwa, baada ya siku tatu atafufuka.

Hakusema kuwa siku za baadaye, siku moja atazaliwa upya. (Nani angejua kama kweli alifanya hivyo?)

Photo of a smiling young woman to illustrate that in Christianity there is not the burden to earn God's acceptance.Nguvu ya Yesu ilifanya miujiza iliyojulikana sana, waliomsulubisha waliweka walinzi katika mlango wa njia inayoenda kwenye kaburi la Yesu, ili walilinde salama.

Pamoja na hayo, siku ile ya tatu, kaburi la Yesu lilikutwa wazi na watu wengi walishuhudia kuwa wamemuona akiwa hai tena.

Habari zikaenenea kote kote ulimwenguni kwa mtu yeyote, Yesu anaweza kabisa kumsamehe dhambi zake na kumjua kuwa atampa uzima wa milele anapomuamini. Ujumbe huu ulikuwa unaeleweka.

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”7

(Kujua zaidi kuhusu Yesu tazama Kwa nini Yesu ni Mungu.)

Yesu anatupa kuhusiana naye na uzima wa milele.

Tofauti na dini nyingi duniani…

Mungu anatualika twende kwake kwa uhuru. Huku si kujidhatiti kama njia ya kujiboresha kama vile kufuata Njia Kuu Nane au Nguzo Tano, au kutafakari, au kazi nzuri au kutii amri kumi za Mungu.

Hizi zinaonekana wazi, zimefafanuliwa vyema, njia za kiroho rahisi kuzifuata. Lakini zinakuwa nzito kuzifuata kikamilifu, na uku muunganiko na Mungu bado uko mbali. Jitiada za dini au matendo mema hayatoshi kufunika dhambi zetu.

Badala yake, tukimjua Yesu kama Mwokozi wetu ambaye kabisa anatupokea kwa sababu alifia dhambi zetu na imani zetu kwake.

Sio dini kuwa na uhusiano na Mungu.

Anakukaribisha ili umjue. Swali ni je, unataka kuwa na uhusiano na Mungu?

Ikiwa ni hivyo, unaweza ukaanza uhusiano na Mungu sasa hivi. Ni rahisi sana, ukimuomba kwa dhati mwenye dhamiri safi kwamba akusamehe dhambi zako na umwalike aingie katika maisha yako.

Photo of a smiling young woman to illustrate that in Christianity there is not the burden to earn God's acceptance.Yesu alisema, “Tazama, nasimama mlangoni [moyoni mwako], nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake.”8

Unaweza kufungua mlango na umkaribishe aje katika maisha yako sasa hivi, tu kwa kumuomba katika maombi. Maneno halisi sio muhimu, lakini hii inaweza kukusaidia kujieleza kwake:

“Mungu, ninakuomba unisamehe dhambi na ninakualika uingie moyoni mwangu sasa hivi. Asante, kwa kufia dhambi zangu. Njoo katika maisha yangu kama ulivyoyatoa. Asante kwa kunipa uhusiano wa milele na wewe.”

Kama umemuomba Mungu aingie katika maisha yako sasa hivi, umeanza uhusiano wako binafsi na yeye. Unaweza kuongea na yeye na yeye atakuongoza katika maisha yako sasa. Tofauti na dini za ulimwenguni, Yesu hakuelekezi kwenye njia ya falsafa, au desturi, lakini anakutaka wewe binafsi umjue na uujue upendo wake kwako.

Hivi ndivyo unavyoweza kukua katika uhusiano wako mpya na Mungu:

 Nilimpokea Yesu maishani mwangu (ujumbe muhimu unafuata)…
 Ninaweza kutaka kumuuliza Yesu maishani mwangu, tafadhali eleza hili kikamilifu zaidi…
 Nina swali…

[na Dkt. Marilyn Adamson]

Maelezo ya chini: (1) Erwin W. Lutzer, Christ Among Other Gods (Chicago: Moody Press,1994), p. 63 (2) Isaya 53:6 (3) Yohana 1:29 (4) Mathayo 26:28 (5) Isaya 53:5, 10, 12 (6) 1Yohana 3:16 (7) Yohana 3:16 (8) Ufunuo 3:20


SHIRIKISHA WENGINE
WhatsApp Share Facebook Share Twitter Share Share by Email More