×
TAFUTA
Mahali Salama pa Kuchunguza Maswali
 jinsi unavyoweza kumjua Mungu
Kuunganishwa na Mungu

Je, Unaweza Kufafanua Utatu Mtakatifu?

Makala ifuatayo inaelezea kwa uwazi na kwa ufupi juu ya Utatu … Je, miungu watatu au mmoja?

WhatsApp Share Facebook Share Twitter Share Share by Email More PDF

Sikiliza makala hii:

Wewe na mimi tunaishi katika ulimwengu wa pande tatu. Vitu vyote vya kimwili vina urefu, upana na kina fulani. Mtu mmoja anaweza kuonekana kama mtu mwingine, au kuishi kama mtu mwingine, au hata kusikika kama mtu mwingine. Lakini mtu hawezi kuwa sawa na mtu mwingine. Wao ni watu binafsi tofauti.

Mungu, hata hivyo, anaishi bila mipaka ya ulimwengu mwenye sura tatu. Yeye ni roho. Na yeye hana mwisho na ni zaidi ya sisi tulivyo.

Ndiyo maana Yesu Mwana anaweza kuwa tofauti na Baba. Na, bado akawa sawa naye.

Biblia inazungumza waziwazi kuhusu: Mungu Mwana, Mungu Baba, na Mungu Roho Mtakatifu. Lakini inasisitiza kwamba kuna Mungu MMOJA tu.

Ikiwa tungetumia hesabu, haingekuwa, 1+1+1=3. Itakuwa 1x1x1=1. Mungu ni Mungu wa Utatu.

Hivyo neno: "Tri" maana yake tatu, na "Umoja" maana moja, Utatu+Umoja = Utatu. Ni njia ya kukiri kile ambacho Biblia inatufunulia kuhusu Mungu, kwamba Mungu bado ni "Nafsi" tatu ambazo zina asili sawa ya uungu.

Wengine wamejaribu kutoa vielelezo vya wanadamu kwa Utatu, kama vile H2O kuwa maji, barafu na mvuke (zote ni aina tofauti, lakini zote ni H2O). Kielelezo kingine kingekuwa jua. Kutoka humo tunapokea mwanga, joto na mionzi. Vipengele vitatu tofauti, lakini jua moja tu.

Hakuna kielelezo kitakachokamilika.

Lakini tangu mwanzo tunamwona Mungu kama Utatu. Katika kitabu cha Mwanzo, kitabu cha kwanza katika Biblia, Mungu anasema, “Na tumfanye mtu kwa mfano wetu…mwanamume na mwanamke aliwaumba.”1 Unaona hapa mchanganyiko wa viwakilishi vya wingi na umoja.

Musa alipomwomba Mungu jina lake, Mungu alijibu, “Mimi ndiye” – aliyepo milele.

Yesu alitumia msemo huo mara nyingi.
“Mimi ndimi nuru ya ulimwengu...”
“Mimi ndimi mkate wa uzima...”
“Mimi ndimi njia, na kweli na uzima. mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi.”

Abrahamu ni mtu anayetajwa katika Mwanzo, maelfu ya miaka kabla ya Yesu kuja duniani. Hata hivyo, Yesu alisema juu yake mwenyewe, “Kabla Abrahamu hajazaliwa, mimi niko.” Wayahudi walielewa kikamilifu kile ambacho Yesu alikuwa akisema kwa sababu waliokota mawe ili wamuue kwa sababu ya “kufuru” - wakidai kuwa Mungu.2 Yesu amekuwepo siku zote.

Hii ilikuja mara kwa mara. Yesu alikuwa wazi sana kuhusu uhusiano wake wa pekee na Baba. Hii ndiyo sababu, “viongozi wa Kiyahudi walijitahidi zaidi kutafuta njia ya kumwua. Kwa maana hakuivunja Sabato tu, bali alimwita Mungu Baba yake, na hivyo akijifanya sawa na Mungu.”3

Kwa umilele wote, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu daima wamekuwa katika uhusiano na mawasiliano wao kwa wao, lakini si kama miungu watatu…kama Mungu mmoja.

“Nafsi zote tatu katika Utatu zina majina ya uhusiano. Mtu wa Kwanza katika Utatu anaitwa Baba. Huwezi kuitwa Baba usipokuwa na mtoto. Na vivyo hivyo kwa Nafsi ya Pili katika Utatu. Huwezi kuitwa Mwana isipokuwa una Baba. Nafsi ya Tatu katika Utatu inaitwa Roho wa Baba (Mt 10:20) na Roho ya Mwana (Gal 4:4-6).”4

Hii inajibu swali:

Ikiwa Yesu ni Mungu, alikuwa akiomba kwa nani?

Akiwa duniani, Yesu aliendelea kuzungumza na Baba, na Baba na Roho waliendelea kuwasiliana naye.

Ingawa si orodha iliyo kamilika, hapa kuna Maandiko mengine yanayoonyesha Mungu ni mmoja, katika Utatu:

  • "Sikia, Israeli! BWANA ndiye Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja!"5

  • “Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu.”6

  • Hakuna Mungu ila mmoja.7

  • Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.”8

  • "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu."9

  • Yesu alisema: “Mimi na Baba tu umoja.”10

  • “Yeye aliyeniona mimi amemwona Baba.”11

  • “Anayenitazama Mimi anamwona yule aliyenituma.”12

  • Mtu ye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.13

  • “Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu mke wako, kwa maana mimba yake ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.”14

  • Malaika akajibu, akamwambia [Mariamu], “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; na kwa sababu hiyo mzao mtakatifu ataitwa Mwana wa Mungu.”15

  • [Yesu akizungumza na wanafunzi wake] “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumjui. yeye, bali ninyi mnamjua kwa sababu anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.” ... “Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.”16

Tafadhali tazama Kwa nini Yesu ni Mungu akitoa ushahidi wa Yesu kuwa Mungu.

 Jinsi ya kuanza uhusiano na Mungu
 Nina swali…

Maelezo ya Chini: (1) Mwanzo 1:26, 27 (2) Yohana 8:56-59 (3) Yohana 5:16-18 (4) Barry Adams, Ufalme ni wa Watoto Wadogo, ukurasa wa 40. (Barry Adams, The Kingdom Belongs to Little Children, page 40.) (5) Kum. 6:4 (6) Isa. 45:5 (7) 1Kor. 8:4 (8)Mt.3:16-17 (9) Mt. 28:19 (10) Yoh. 10:30 (11) Yoh. 14:9 (12) Yoh.12:45 (13) Rum. 8:9 (14)Mt.1:20 (15) Luka 1:35 (16) Yohana 14:16-17, 23


SHIRIKISHA WENGINE
WhatsApp Share Facebook Share Twitter Share Share by Email More